28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mata alimtaka Pique kurudi Man United

JuanMata_3177063MANCHESTER, ENGLAND

NYOTA wa klabu ya Manchester United, Juan Mata, ameweka wazi kwamba alimshawishi beki wa Barcelona, Gerard Pique, kurudi katika timu yake ya zamani Man United.

Wachezaji hao wa timu ya Taifa ya Hispania wamekuwa na uhusiano wa karibu ambapo Mata alitumia nafasi hiyo kumshawishi Pique lakini alishindwa.

“Nimekuwa na Pique kwa muda mrefu tangu tukiwa wadogo, lakini nilijaribu kumshawishi aweze kurudi Manchester United, ila ilikuwa ngumu, anadai kwamba bado anaipenda sana Barcelona,” alisema Mata.

Pique aliwahi kuwa mchezaji wa Manchester United kwa miaka minne baada ya kuondoka Barcelona, huku akiwa na umri wa miaka 17, lakini alirudi tena Barcelona mwaka 2008, ambapo hadi sasa bado anakipiga katika klabu hiyo.

Lakini uongozi wa klabu ya Barcelona kwa sasa umedai kwamba una mpango wa kusajili beki kwa kuwa wachezaji wa safu hiyo umri wao unaonekana kuwatupa mkono.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles