27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Odinga agoma kuachana na siasa

NAIROBI,Kenya

KIONGOZI  wa upinzani chini hapa, Raila Odinga, amesema hana mpango wa kuachana na siasa hivi karibuni licha ya kukabidhiwa wadhifa mkubwa katika Umoja wa Nchi za  Afrika (AU).

Odinga aliyasema hayo juzi akiwa wilayani Yimbo na akawataka wanamtaka kuachana na siasa  baada ya kupata uteuzi huo kutopoteza muda wao na badala yake watafute kazi nyingine ya kufanya.

“Ningependa kufafanua kwamba uteuzo wangu wa hivi karibuni hautaathiri shughuli zangu za siasa,” Odinga aliwaambia waombolezaji wakati wa mazishi ya  William Odhiambo Okello.

“Hivyo nashauri kuachwa  mjadala  juu ya hatma yangu katika siasa,”aliongeza kiongozi huyo mkuu wa upinzani.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Odinga alichaguliwa kuwa Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Afrika kuhusu miundombinu wadhifa ambao ni mkubwa kidiplomasia  katika Umoja huo.

Uteuzi huo ndiyo uliwasukuma wabunge wengi kutoka Mkoa wa Mlima Kenya kumtaka kiongozi huyo kuachana na siasa za nchini hapa.

Uteuzi huo pia umekuja wakati nchi hii imeshaanza mjadala nani atakuwa mrithi wa Rais Uhuru Kenyatta kutoka upande wa vyama vya upinzani na chama tawala cha  Jubilee.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari,   kambi ya Makamu wa Rais William Ruto inaeleza kwamba uteuzi  huo  unaweza kumzuia  Raila kuingia tena katika mbio za kuwania kiti cha urais na hivyo mwaka 2022 kumnufaisha Ruto.

Hali hiyo pia inaripotiwa kuwaacha njia panda washirika na wafuasi wake ambao wamekuwa wakikuna vichwa wakihoji kama  nafasi hiyo itamruhusu aendelee na shughuli za siasa, jambo ambalo aliamua kuliweka wazi.

“Hata kama nitakuwa nikizunguka kwenye miji mkuu yote ya nchi za Afrika ngome yangu kuu itakuwa ni  Nairobi. Sitakwenda mahali popote,”alifafanua kiongozi huyo.

“Nafikiri wale wote wanaodhani nitaachana na siasa wanaota ndoto za mchana,”aliongeza Odinga.

Alisema  viongozi wa Chama Cha NASA  walishajitolea mengi katika ukombozi wa taifa hili na hivyo wanapaswa kuyaendeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles