|Washington, Marekani
Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa upinzani Seneta John McCain, aliyafariki dunia jana Jumamosi Agosti 25 kwa saratani ya ubongo.
Katika taarifa yake aliyoituma pamoja na mkewe Michele, Obama ameelezea kuwa yeye na McCain wametokea katika vizazi na historia tofauti lakini walishindana katika kinyang’anyiro cha juu cha siasa nchini Marekani.
Amesema waliona mapambano ya kisiasa, hata kama kulikuwa na upendeleo wa kitu kama cheo ila walipata nafasi ya kuonesha maadili nyumbani na duniani kote na kwamba waliona Marekani kama sehemu ambayo kila kitu kinawezekana kuwa raia wa kizalendo ni wajibu wao na kuhakikisha inabaki hivyo milele.
“Wachache wetu wamejaribiwa kama alivyojaribiwa John na kuonesha ujasiri wa aina yake kama alivofanya, lakini sote sisi tunamani kuwa na ujasiri kama huo ili kufanya zaidi ya vitu vyetu na yeye, ametuonesha ni namna gani hii ina maana na katika hili wote tuna deni.
“Mimi na Michelle kwa dhati ya mioyo yetu tunatuma salamu za rambirambi kwa Cindy na familia yote,” imesema taarifa hiyo ya Obama.