Nyota wa muziki Malawi afariki dunia

0
799

Grace-ChingaNYASA, MALAWI

MSANII wa muziki wa injili nchini Malawi, Grace Chinga, amefariki dunia juzi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kichwa.

Rafiki wa karibu wa familia ya marehemu Grace, Pasta Chris Suya, aliliambia gazeti la Nyasa Times la nchini humo kwamba, mwanamuziki huyo alikimbizwa hospitalini baada ya kulalamikia maumivu makali ya kichwa.

“Tulipokea simu kwamba alikuwa anasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa na tukakimbia hadi kwake kwa mwendo wa saa moja, baada ya kufika tulimpeleka hospitali ya Queens Elizabeth lakini alifariki dunia,” alisema Suya.

Katika akaunti ya facebook ya marehemu Grace, siku chache zilizopita alitangaza kwamba anatarajia kuachia albamu yake mpya hivi karibuni lakini ndoto hizo zimezimika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here