31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kleyah azindua ‘The African Drum’, Jay Dee ‘Naamka tena’

Untitled-1NA FESTO POLEA

USIKU wa kuamkia jana ulikuwa wa kihistoria kwa wanadada wawili, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ na Claire Pamela Kamahoro ‘Kleyah’ ambao wote walizindua kazi zao mpya katika muziki wanaoufanya.

‘Kleyah’ ambaye ndiye mkali wa wimbo wa ‘Msobe Msobe’ aliomshirikisha Barnaba Boy, alizindua video ya wimbo wake mpya wa ‘The African Drum’ katika Hoteli ya Hyatt Regency ‘Kilimanjaro’ huku Jay Dee akizindua ‘Naamka tena’.

Wimbo huo wa Kleyah wenye mahadhi ya Afro pop umetayarishwa na prodyuza Nahreel na video imeandaliwa na Justin Campos. Umeonyesha namna ambavyo maisha ya Waafrika yalivyo na uzuri wa kujivunia wa Mwafrika.

Kabla ya kuiona video hiyo, Kleyah akiwa na wanenguaji wake walionyesha umahiri wa kucheza wimbo wote kwa kutumia minyumbuiko ya kila namna kiasi kwamba kila aliyehudhuria katika uzinduzi huo aliburudika.

Baada ya shoo hiyo ya moja kwa moja ndipo uzinduzi wa video hiyo ulipoanza ikionyesha madhari nzuri zilizotumiwa na mwongozaji huku Kleyah na wanenguaji wake wakitumia vema vipaji vyao vya unyumbulikaji.

Video hiyo itaanza kuonyeshwa kwenye mitandao na vituo mbalimbali vya redio na runinga baada ya kuachiwa rasmi leo na kituo maarufu cha MTV.

Baada ya uzinduzi ulioongozwa na mwanadada kutoka Marekani akisaidiana na Sudi Brown wa Clouds Fm waliokuwa wakinogesha vema uzinduzi huo alisema video hiyo ni maandalizi tosha ya kuelekea albamu yake inayokuja siku zijazo.

“Mimi napenda vitu vizuri, huu wimbo wangu nimeufanya kwa ubora na video pia kwa kuwa nataka wasanii waige tunakotakiwa kwenda lakini haya ni maandalizi ya albamu yangu nitakayoitoa baada ya kukamilisha nyimbo nizitakazo ambazo nitarekodi na wasanii wakubwa wa hapa Bongo,” alieleza Kleyah.

Kabla ya kuzindua wimbo huo wa ‘The African Drum’, Kleyah alishatamba na wimbo wa ‘Msobe Msobe’, ‘Lovers Eyes’ na ‘Don’t Sly me’.

Lady Jay Dee

Jay Dee alikuwa kimya kwa muda mrefu hivyo kampeni yake ya kurudi upya aliianza mapema kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa muziki wakiwemo wanamuziki maarufu, wakurugenzi na watu maarufu ndani na nje ya nchi kwa kutumia kaulimbiu yake ya ‘Nasimamia ninachokiamini, nafanya ninachokipenda, moyo wangu shujaa, naamka tena.”

Jay Dee ameamka sasa wapenzi wa muziki wake mtegemee muziki mzuri kutoka kwake kwa kuwa ameamka tena.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles