26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Ciara, Ashton wafikia pabaya

Ashton WilsonNEW YORK, MAREKANI

BAADA ya msanii wa muziki, Ciara Harris, kutangaza kuwa anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mpenzi wake mpya, Russell Wilson, mke wa zamani wa Wilson amemjia juu msanii huyo.

Wiki iliyopita Ciara na Wilson walivishana pete na wakatangaza kuwa wanatarajia kuoana siku za hivi karibuni, lakini juzi mke wa zamani wa Wilson, Ashton Wilson, amedai kwamba yeye atabaki kuwa mke sahihi wa Wilson.

Wilson na Ashton walianza uhusiano wao tangu wakiwa shule na wakafanikiwa kufunga ndoa mwaka 2012, lakini walikuja kuachana 2014, ambapo Wilson akaamua kutoka na Ciara, lakini Ashton anaamini bado ana uhusiano na mume huyo wa zamani.

“Ciara anajisumbua, anajua wapi nilikotoka na Wilson, lakini nashangaa kuona wanavishana pete hakuna kitu ambacho kitaendelea,” aliandika Ashton.

Hata hivyo, Ciara naye alijibu kupitia akaunti yake ya twitter na kuandika: “Ninaamini tayari nimemaliza,” aliandika Ciara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles