MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Peter Msechu, amesema nyimbo 10 alizokuwa akiziandaa pamoja na video zake ndizo zinazomfanya awe kimya kimuziki.
“Nimekuwa kimya kwa muda mrefu kwa kuwa nilikuwa najipanga kuachia ngoma zangu mpya ambazo kwa sasa ndiyo namalizia video zake.
“Nimeshatimiza nyimbo 10 ambazo zipo katika hatua ya mwisho kukamilisha video zake hivyo mashabiki wangu wakae tayari kupokea kazi nyingi zenye ubora wa kutosha kutoka kwangu,” alieleza Msechu.
Peter Msechu kwa sasa anashughulika na ukuzaji wa vipaji vya wasanii Wilaya ya Kinondoni.