24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Nyasi U/Taifa zamkera Kerr

dylanker-haiphongNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amesema wachezaji wake walicheza vizuri dhidi ya Azam FC juzi licha ya kukosa mabao mengi ya wazi yaliyowanyima ushindi na kudai kuwa timu hiyo ilitakiwa kufunga mabao manne kipindi cha kwanza.

Simba wanaoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, juzi walilazimishwa sare ya 2-2 na vinara wa ligi hiyo Azam katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwingereza huyo alisema jambo jingine lililowafanya washindwe kucheza kwa kasi yao ni namna Uwanja wa Taifa ulivyo kwani hauruhusu kucheza soka la aina hiyo kutokana na nyasi zake kutokatwa vizuri.

Alisema kuwa wachezaji wake walikuwa wakisubiri mpira kwa muda mrefu pale wanapopigiana pasi za haraka lakini ilishindikana kutokana na hali ya uwanja.

“Pia naweza kukubali kuwa maandalizi ya timu ya Taifa yaliathiri timu, sisi tulikuwa na wachezaji 10, Jjuuko (Murshid) alirejea juzi, lakini ukubwa wa kikosi ulisaidia kuondoa hilo kwani niliwaambia wachezaji waliobakia waonyeshe kiwango cha juu kuliko wale waliokuwa timu za Taifa.

“Tulivyokuwa kambini Zanzibar tulicheza kwenye kapeti (uwanja wa nyasi bandia), mpira ulikuwa ukienda safi na tulicheza

kwa kasi yetu, lakini hapa sijui kwa nini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshindwa kurekebisha hilo.

“Katika ligi kubwa duniani na hata hapa Afrika viwanja vimekuwa vikiwekwa katika hali nzuri sijui kwanini jambo hili hapa haliangaliwi,” alisema.

Simba inatarajiwa kushuka tena  dimbani keshokutwa kucheza mechi ya kiporo dhidi ya Ndanda FC katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara mchezo ambao awali haukufanyika kwenye raundi ya sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles