Nora: Wanaonitaka kimapenzi hukimbia ndoa

0
1603

NORANA RHOBI CHACHA

MSANII wa Filamu za Bongo, Nuru Nasoro ‘Nora’ amefunguka kwamba wanaume wengi wanaomtaka kimapenzi humkimbia anapowataka wasubiri hadi watakapofunga ndoa.

Nora alisema ameweka sharti hilo ili ampate mwanamume wa kweli, lakini anaona kama amejiwekea gundu kwa kuwa wengi waliojitokeza kwake hukimbia anapowaeleza masuala ya kusubiri hadi ndoa.

“Si kwamba sitongozwi, natongozwa tena wengi wanakuja kwa gia ya kutaka kunioa, lakini kila mwanamume anataka kushiriki tendo la ndoa kwanza ndipo atangaze ndoa, nami nataka ndoa kwanza ndipo mapenzi maana nilishaolewa na kuachika mara mbili, kwa sasa nataka mwanamume wa kweli atakayenipenda mimi na mapenzi yangu si ujanja ujanja wa wanaume,’’ alieleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here