27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Kaka wa Jenerali Mwamunyange naye akanusha mdogo wake kulishwa sumu

Davis MwamunyangeNa Victoria Patrick, Dar es Salaam

KAMISHINA Msadizi na Mwandamizi  mstaafu wa Jeshi la Polisi, Aden Mwamunyange ambaye ni kaka wa Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange, naye amekanusha taarifa   zilizoenezwa hivi karibuni katika mitandao ya  jamii kuwa amelishwa simu.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Jeti Lumo,  Dar es Salaam jana, alisema hizo taarifa hizo si za kweli na ni uzushi.

“Mimi kama mwana familia nakanusha taarifa hizo zinazosambaa mitandaoni, habari hizo hazina ukweli hata kidogo.

“Jenerali Mwamunyange ni mzima wa afya,  anaendelea na shughuli zake kama kawaida   na yuko nje ya nchi kwa safari za kazi,” alisema Aden.

Alisema ni kawaida kwa Jenerali   Mwamunyange kumuaga kila anaposafiri na kama kaka yake alimuaga kuwa alikuwa anasafiri kikazi kwenda nje akianzia   Italia.

Pia alikanusha taarifa zilizosema kuwa ukoo wao umepewa fedha   kuzima taarifa za Jenerali Mwamunyange na akawataka wananchi kuzipuuza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles