27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Linnah: Mpenzi wangu hataki picha za mitandaoni

linah...NA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga ‘Linnah’ amefafanua kwamba haweki picha za mpenzi wake kwenye kurasa zake za mitandaoni kwa kuwa mpenzi wake huyo hataki na si kwamba wameachana.

Linnah alieleza kwamba yeye na mpenzi wake huyo raia wa Uganda, Williams Bugeme, wamekubaliana waache utaratibu huo wa kuweka picha zao kwenye mitandao ya kijamii na si kwamba wameachana kama wengi wanavyodhani,

“Bado nipo na Williams, wengi wameshangaa kwa nini siku hizi siweki picha nikiwa naye kama nilivyokuwa nafanya hapo zamani, penzi letu bado lipo imara, lakini tumekubaliana tu kwamba tuache kuyaweka hadharani mapenzi yetu,” alisema Linnah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles