MKALI wa wimbo wa ‘Wanajishuku’ aliomshirikisha Dj Pierra Makena na Chege kutoka Tanzania, Hubert Nakitare ‘Nonini’ wa Kenya, ametumia kiasi kikubwa cha fedha zake kununua nguo na miwani kwa ajili ya kuwasaidia albino.
Hata hivyo, msanii huyo amewataka wasanii wenzake na watu maarufu wajitokeze kuwasaidia walemavu badala ya kutumia fedha zao katika matukio ya ulevi na anasa nyingine.
“Watu maarufu wanatakiwa wajitolee kwa jamii zao, wakiwemo walemavu, si kutumia fedha zao kwa mambo yasiyo na msingi,” alisema Nonini.