28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

NOFIA yatakiwa kuanzisha kitengo cha masoko

Na Safina Sarwatt, Moshi

Serikali imeutaka umoja wa wenye viwanda vya mazao ya misitu Kanda ya Kaskazini (NOFIA), kuanzishia kitengo cha masoko kitakachowasaidia kujitangaza na kupata masoko ya uhakika nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 16, na Naibu Kamishna wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini (TFS), Edgar Masunga wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 11 wa wana viwanda wadogo na wakati wanaochakata mazao yatokanayo misitu Kanda ya Kaskazini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa YMCA mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

“NOFIA anzisheni kitenge cha soko na msingoje serikali iwatafutie masoko, angalieni mfano kwa wenzenu wa sekta ya utalii ambao wamekuwa wakitafuta masoko yao na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupata masoko mengi.

“Kitengo cha masoko ni muhimu kitasaidia kutangaza bishara, kupata uhakika wa soko ndani na nje nakuongeza pato la wafanyabishara wa mazao ya msitu,” amesema Masunga.

Aidha, Masunga ameutaka umoja huo kuhakikisha kwamba unazingatia ubora wa uchakataji wa mazao hayo ili kuweza kushindana katika masoko.

“Kumekuwepo na mazao ya misitu yasiyo na ubora kuingizwa sokoni, yakitoka kwenye mashamba, hivyo zingatieni ubora wa uchakati ili muweze kuingia kwenye ushindani wa masoko,” amesema Masunga.

Awali Mwenyekiti wa (NOFIA), Mhandisi Frank Karonge aliiomba serikali kuweka mazingira bora ya kusaidia vijiji, shule na taasisi za dini zinazozunguka misitu ya kupandwa ili zifaidike kwa kupewa mbao badala ya magogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles