33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Redcross wajaza nafasi za uongozi Manyara

Na Mohamed Hamad, Manyara

Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Tanzania Redcross Society) Mkoa wa Manyara, kimekamilisha kujaza safu za uongozi katika nafasi mbalimbali watakao watumikia wananchi na shirika hilo kwa miaka mitano ijayo.

Waliojaza nafasi hizo ni Makamu Mwenyekiti, Theresia Chales, Mratibu, Ernest Mbuta, Mweka hazina, Benard Laiza, Meneja Miradi, Haruni Mvungi na Sinda Sungwa Mipango na Maendeleo.

Wajumbe wa mkutano mkuu wa Tanzania Redcross Society Mkoa wa Manyara, katika picha ya pamoja baada ya kufanya uchaguzi kujaza nafazi tano zilizokuwa wazi.

Wengine ni, Mwenyekiti wa Vijana, Jacob Mollel, Mjumbe wa kuteueliwa, Mhandisi. Elipid Tesha na Kitengo cha Habari na Maafa, Mohamed Hamad.

Mkutano Mkuu wa Shirika umefanyika mjini Babati, chini ya Mwenyekiti wa Tanzania Redcross Mkoa wa Manyara, Wakili Moses Basila, ambaye alitaja idadi ya nafasi zilizokuwa wazi na ambazo zimejazwa na viongozi kwa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu.

Wakili Basila amesema kupatikana kwa viongozi hao kutatoa mwelekeo wa shirika hilo kutekeleza mipango yake ya miaka mitano ambayo itakuwa na tija kubwa kwa shirika na kwa wananchi mkoani humo.

Ameyataja malengo ya TRCS Manyara kuhakikisha shirika linakuwa na Ofisi ya Mkoa, kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato, kuongeza idadi ya wanachama wapya 33,0000 kwa miaka mitano kama lilivyo lengo la Taifa kuongeza wanachama wapya 1,000,000.

Malengo mengine ni kuwa na miradi mipya na kusimamia kikamilifu iliyopo chini ya wahisani ili kuleta tija, kuwa na vikundi vinavyozalisha ndani ya matawi pamoja na kuimarisha baraza la vijana.

pia kuna kuimarisha mabaraza ya vijana kuanzia kwenye matawi wilaya na Mkoa ambayo yatakuwa na jukumu kubwa kuhakikisha masuala mbalimbali ya Tanzania Redcross Society inapunguza ama kuondoa maumivu yanapojitokeza maafa.

Kwa upande wake, Theresia Chales aliyechaguliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa Tanzania Redcross Society Mkoa wa Manyara, ameahidi wajumbe wa mkutano mkuu kuwa atahakikisha anatimiza wajibu wake kama ilivyo katika kanuni saba za Redcross.

“Kuchaguliwa ni jambo moja, utekelezaji ni jambo lingine…nitakuwa na jukumu kubwa kuhakikisha nashirikiana na wenzangu kufikia malengo ya Tanzania Redcross ambayo ni kupunguza au kuondoa maumivu kwa wahanga,” amesema Theresia.

Upande wake, Christopher Nzala mwezeshaji wa mafunzo kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Tanzania Redcross amesema, Redcross ni kusaidia cha serikali kutimiza majukumu yake kuhudumia wananchi ambapo ametaja kanuni saba za Redcross kuwa ni pamoja na ubinadamu, uadilifu, uhuru, kujitolea, umoja na hadhi sawa.

Amesema mwanachama akifahamu kanuni hizo atafanya kazi kwa uadilifu, uaminifu mkubwa bila mawaa huku akiwataka kuzingatia kanuni ya tano, kujitolea ambayo ndio nguzo kuu ya Redcross katika kuwatumikia wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles