28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Baraza la Madiwani Makete lagoma kupokea ripoti

Na Mwandishi Wetu, Makete

Baraza la madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Makete Mkoani Njombe limegoma kupokea ripoti ya utendaji kazi wa halmashauri hiyo kwasababu ya kukosa muda wa kuisoma vizuri na kuipitia ripoti hiyo ili waweze kujiridhisha kama fedha zilizotumika ni sawa na miradi inayoonekana kwenye ripoti hiyo.

Hayo yametokea leo Desemba 17, baada ya madiwani hao kupewa ripoti hiyo baada ya kuapa kutoka kwa Mkurugenzi wa halmashauri na kuwataka waipokee na kupitisha huku wao madiwani wakidai kutokana na Mwongozo uliotolewa na TAMISEMI ikiwataka wapate siku saba kabla kwa kuisoma ndio wajadili na kuipitisha taarifa hiyo.

Mbunge wa jimbo la Makete, Festo Sanga(kulia) akichangia hoja katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Makete.

Baadhi ya madiwani hao wakiongozwa na mbunge wa jimbo hilo, Festo Sanga wamesema hawawezi ipitisha kwani kuna baadhi ya miradi wanaitilia shaka bajeti zake hivyo wanataka kupitia kifungu kwa kifungu kupitisha ripoti hiyo.

Akichangia wakati wa kikao hicho Sanga alisema kuwa serikali imetoa mwongozo wa diwani anatakiwa apate taarifa siku sana kabla ya kikao ili apate muda wa kuipitia hiyo taarifa vizuri na kuona yale yaliyoandikwa kwenye taarifa yapo kwenye kata yake au hayapo.

“Hatuwezi ijadili hii taarifa haraka haraka leo na kuipokea wakati hatujaisoma vizuri haya makabrasha tumekutana nayo hapa hapa ukumbini,tutakuwa hatujawatendea haki wananchi wa makete.

“Leo tuhairishe kikao turudi nyumbani tukasome vizuri hii taarifa ili tukija tupoker au tupitishe viti tunavyovijua kila mtu apitie kwenye kata yake aone kama fedha zililetwa,zimelipwa au hazijalipwa ili tupokee kitu kizuri na tujadili kitu tunachokifahamu,” amesema Sanga.

Baraza hilo lipo chini ya mwenyekiti wake wa halmashauri, Francis Chaula wamepitisha kwa kauli moja kesho wataijadili ripoti hiyo na kuipitisha kama itafaa na kukosoa pale ambapo fedha zimetumika vibaya.

Baraza hilo linaongozwa na madiwani hao wote kutoka chama kimoja Chama cha mapinduzi(CCM).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles