23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

NMB Zanzibar yakabidhi mabati 200 na vifaa vya ukarabati wa madarasa

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Benki ya NMB Tawi la Zanzibar imekabidhi mabati 200 na vifaa vyengine vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa ya shule ya sekondari ya Jambiani, Kusini Unguja.

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Donatus Richard (wapili kulia) akipeana mkono na Waziri wa Kilimo Mali asili na umwagiliaji Zanzibar, Soud Nahoda Hassan wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi vikiwemo mabati mia mbili kutoka benki ya NMB kwa ajili ya shule ya Jambiani Sekondari.

Akizungumza katika hafla ya makabidhianao hayo iliyofanyika skulini hapo, Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alisema wameamua kutoa msaada huo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu.

“Benki ya NMB tumeamua kushirikiana pamoja na Jamii yote inayozunguka eneo la Jambiani kuchangia mabati 200 kwa ajili ya kutatua changamoto ya kuvuja kwa madarasa wakati wa mvua,” alisema Donartus.

Aliongeza kuwa elimu ni kichocheo cha maendeleo hivyo kuna kila sababu kwa watoto kupata mazingira mazuri ya kupata elimu na kusisitiza ndio maana benki ya NMB imeamua kuisaidia skuli hiyo.

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Paje ambae pia ni Waziri wa Kilimo, Uvuvi, Mifugo na Umwagiliaji, Sudi Nahoda, ameishukuru benki hiyo kwa msaada huo na kusema utasaidia kutatua changamoto ya kuvuja kwa skuli hiyo.

“Nikuhakikishieni kuwa msaada huu mliotupatia una thamani kubwa na kiuhalisia NMB ni moja kati ya mashirika yanayojali Jamii katika kuleta maendeleo,” alisema Sudi.

Kwa upande wake kaimu mwalimu Mkuu wa Skuli ya Jambiani, Haji Haji ameishukuru NMB kwa msaasa huo, amesema kwa muda sasa wamekuwa wakikabiliwa na ubovu wa madarasa ambapo wanafunzi wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo  katika vipindi vya mvua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles