29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mama Lishe watakiwa kiuzingatia usafi wa mazingira

Na Sheila  Katikula, Mwanza

Wafanyabiashara wa Chakula maarufu kama Mama Lishe na Baba Lishe katika kata ya Pamba iliyopo jijini Mwanza wametakiwa kuzingatia kanuni za utunzaji wa mazingira kwa kuweka  mabaki ya chakula  kwenye vyombo maalum na siyo kutupa ovyo barabarani.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz , Mtendaji wa Kata ya Pamba, Jonas Mugisha, amesema kila mama lishe anapaswa kutupa taka taka za mabaki kwenye vyombo maalum na siyo  kuzitupa  ovyo barabarani kwani kufanya hivyo ni kukiuka miongozo ya usafi wa mazingira.

Amesema Mamlaka zimejipanga kuwachukulia hatua wote wanaokiuka kanuni, miongozo na sheria za usafi wa mazingira ili iwe fundisho kwa wengine wanaovunja na kusisitiza kila mama lishe anapaswa  kuvaa sare  walizoagizwa na maafisa afya ili kuwa katika hali ya usafi.

“Nawaomba mama lishe wote wafuate sheria zilizowekwa ikiwamo kuweka uchafu kwenye vyombo  maalum ili kuepuka kutupa  taka taka ovyo na kuchafua mazingira, kuvaa sare wakati wa kuhudumia wateja  na vile vile  tutaweka mgambo kila sehemu ili wakamate wanaovunja sheria na tutaendelea  kukagua kwa mama ntilie wote,” amesema Mugisha.

Naye, Ofisa Afya wa  Jiji la Mwanza, Sophia kiluvia, amesema ili kuepuka magonjwa ya mlipuko  kila mmoja anapaswa kufuata taratibu za kiafya kwa kuacha kutupa taka ovyo kwani kwenda kinyume na sheria zilizowekwa ni kosa na  hatua kali zitachukuliwa ili  iwe fundisho kwa wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles