27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yaendelea kuwajaza wateja mamilioni

Mwandishi Wetu,Dodoma

Droo ya Mastabata Kivyakovyako inayochezeshwa na BENK ya NMB jana iliingia katika hatua nyingine huku mamilioni ya fedha yakienda kwa wateja.

Siku ya leo Jumatatu Februari 28, imekuwa furaha kwa wateja 25 wa NMB ambao kila mmoja aliibuka na kitita cha Sh milioni 1 kutoka kwenye droo hiyo.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (katikati) akionyesha kadi za benki ambazo Mteja wa NMB akitumia kwenye manunuzi ataingia kwenye droo ya MastaBata ambapo jana,  droo ya mwezi  ilichezeshwa jijini Dodoma. Kulia ni Afisa huduma kwa wateja benki ya NMB, Suzan Manga na kushoto ni Mwakilishi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha Nchini , Ibrahim Shikana.

Mastabata kivyakovyako ni droo inayochezeshwa na Benki ya NMB kwa wateja wanaotumia kadi za Master Card kwa ajili kufanya miamala kwenye ATM, malipo kwenye Posi na QR.

Hadi kufikia leo zaidi ya wateja 800 walishajinyakulia kitita cha Sh 100,000 kwa kila mmoja na ndipo wakaingia katika droo ya pili ya mwezi ambayo inalenga kuwafikia jumla ya watu 50 kwa kiwango hicho huku wengine 30 kuibuka na Sh milioni tatu kila mmoja kwenye droo ya mwisho.

Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki hiyo Nsolo Mlozi alisema jana kuwa washindi wa jana walikuwa katika droo ya mwezi ambayo kila mshindi anaondoka na kitita cha Sh Milioni moja kwenye kampeni hiyo  iliyoanza Desemba 24,2021.

Mlozi alisema washindi hao wataendelea kuchukua zawadi zao hadi droo ya mwisho ya shindano hilo ambalo limetengewa Sh milioni 200 na zote zitawafikia wateja.

“Fedha zilizotengwa ni Sh milioni 200 na zimeshachukuliwa na wateja wengi na bado wanaendelea kuchukua zawadi zao, niwasihi wateja wetu kuendelea kutumia kadi zao ili waendelee kujishindia,” alisema Mlozi.

Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Ibrahim Shikana alisema mchezo huo umekuwa na manufaa kwa wateja na Serikali na kuwa bodi inafurahia uwepo wake.

Shikana alisema kwa namna ilivyo, NMB inaweza kuwa moja ya taasisi za kifedha zinazoaminika zaidi kwenye droo zake kwani hakuna malalamiko yoyote toka kwa wateja wao.

“Kwa michezo mingi wanayochezesha imekuwa ikifuata sheria na kanuni na washindi wanapatikana kihalali lakini Serikali inapata mapato yake, naomba watu waendelee kutumia kadi hizo ili wawe kwenye nafasi ya kushinda,” alisema Shikana.

Hata hivyo ombwe la watu kutokupokea simu jana liliendelea hivyo watu wengi kujikuta wakikosa zawadi zao kwa kutokupokea simu.

Wateja wengi waliokuwa ndani ya benki ya NMB tawi la Dodoma walikusanyanyika kushudia droo hiyo ambapo wengi walifurahi kuwa ilikuwa ikichezwahwa kwa uwazi na haki.

Marius Mazengo alisema hakuwa na taarifa za namna gani huwa wanashinda lakini alivyotazama jana aliona kuwa mchezo huo ni haki.

“Mimi umri wangu umekwenda, mara nyingi siji benki natumia kadi kwa kukwepa foleni, kwa hiyo kumbe nami nipo kwenye orodha ya kushinda na iko siku najua nami nitashinda,” alisema Mazengo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles