25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

NMB Bonge la Mpango yatoa zawadi za Mil 23 kwa mpigo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzani Digital

ILE Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde inayoendeshwa na Benki ya NMB ‘NMB Bonge la Mpango,’ imezidi kushika kasi, baada ya wiki hii kumwaga zawadi zenye thamani ya Sh milioni 23.5 kwa mpigo, hivyo kufanya thamani ya jumla ya zawadi zote kufikia Sh milioni 117 katika kipindi cha wiki 9.

Droo mbili kwa mpigo za ‘NMB Bonge la Mpango – 2merudi Tena,’ zimefanyika Jumatano jijini Dar es Salaam, ikiwamo ya mwisho wa mwezi (Novemba) iliyotoa zawadi za pikipiki tatu za mizigo aina ya Skymark na droo ya wiki ya 9 iliyotoa washindi 12, kati ya hao 10 wakishinda pesa taslimu na wawili wakijinyakulia pikipiki hizo miguu mitatu.

Katika droo hiyo iliyofanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Saleh Omari (wa Tawi la Chakechake), Kelvin Masava (Mwenge) na George Nyaisonga (Mbalizi Road), walitangazwa washindi wa mwisho wa mwezi Novemba wa pikipiki za mizigo zenye thamani ya Sh milioni 4.5 kila moja.

Nao Ludovick Damas (Masasi) na Ally Mnyone (Tawi la Madaraka), waliibuka washindi wa pikipiki mbili za droo ya tisa, iliyotoa pia washindi 10 wa pesa taslimu, wakiwemo Luqman Khamis (Congo Street), Wilfred Rajabu (Mlimani City) na Alberth Fanuely (Madaraka).

Washindi wengine wa pesa taslimu waliopatikana katika droo ya tisa ni pamoja na Ramadhani Maambe (Chalinze), Upendo Israel (Kahama), Rashid Mussa (Lindi), Melkiory Mholya (Songea), Victoria Bunyinyiga (Tarime), Msafiri Daffa (Wami) na Meshack Jonathan (SM-Kenyatta Road).

Aidha, pikipiki tano za mizigo zilizotolewa wiki hii, zinafanya kampeni hiyo hadi sasa kuwa imeshatoa jumla ya pikipiki 24 zenye thamani ya Sh milioni 108 – kati ya pikipiki 50 zitakazotolewa katika kampeni yote, ambako zawadi za pesa taslimu zimefikia Sh milioni 9, hivyo thamani ya jumla ya zawadi zote kufikia Sh milioni 117.

Kwa Sasa NMB Bonge la Mpango imebakisha pikipiki 26 zenye thamani ya Sh milioni 117 zinazoshindaniwa, sambamba na pesa taslimu Sh milioni 3 zitakazoenda kwa washindi 30 wa wiki tatu zilizobaki kuhitimisha kampeni hiyo ambayo ina zawadi zenye thamani ya Sh milioni 237.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles