27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

NKURUNZIZA AZINDUA KAMPENI KUBAKI MADARAKANI HADI 2034

BUJUMBURA, BURUNDI


RAIS Pierre Nkurunziza, amezindua kampeni ya kutaka kufanyika kwa kura ya maoni, ambayo inaonwa kuwa jaribio la kurefusha utawala wake hadi mwaka 2034.

“Hii ni siku ambayo mmekuwa mkiisubiri,” alisema Nkurunziza akiuambia umati wa wafuasi wake katika Wilaya ya Gitega iliyopo katikati ya Burundi juzi, huku akiwatishia wale wanaotaka kukwamisha mpango huo utakaofanyika mapema 2018.

Serikali ilianzisha mchakato wa kurekebisha katiba Oktoba mwaka huu, ambayo iwapo itapitishwa, inaweza kumruhusu Nkurunziza kutumikia mihula mingine miwili ya miaka saba kuanzia 2020 hadi 2034.

“Tunachukua nafasi hii kuwaonya wale wanaotaka kuhujumu mradi huu, iwe kwa maneno au matendo watakuwa wameuvuka mstari mwekundu,” alionya Nkrunzinza.

Kampeni hiyo iliyokuja siku moja baada ya Serikali kuanzisha operesheni ya kuchangisha fedha kwa uchaguzi wa mwaka 2020 licha ya kudaiwa kuwa ya hiari, lakini imelaaniwa na makundi ya haki za binadamu ikielezwa kama mpango wa kijambazi.

Viongozi wa upinzani walio uhamishoni, walisema kura hiyo ya maoni itakuwa ‘mazishi’ kwa mwafaka wa amani uliotiwa saini mwaka 2000.

Mkataba huo wa amani ulisaidia kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa miaka 13 na kusababisha vifo vya watu 300,000.

Burundi ilitumbukia kwenye mzozo mwingine wa kisiasa mwaka 2015 baada ya Nkurunziza kukataa kung’atuka kufuatia kumaliza muhula wake wa pili, badala yake akawania na kushinda muhula wa tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles