24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP, WAZIRI WAKE WAPINGANA KUHUSU KOREA KASKAZINI

WASHINGTON, MAREKANIRAIS Donald Trump wa Marekani na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Rex Tillerson wametofautiana hadharani katika kile kinachoonyesha uwapo wa sintofahamu ya kiuongozi.

Hili linakuja baada ya Tillerson kutoa pendekezo la kuanza mazungumzo ya moja kwa moja na Korea Kaskazini bila ya kuwapo masharti yoyote, kitu ambacho kilipingwa baadaye na Trump.

Hatua hiyo ya Tillerson ilikuwa inaachana na msimamo wa awali wa kuitaka kwanza Korea Kaskazini ikubali kuachana na silaha zake za nyuklia kabla ya mazungumzo kufanyika.

Mbinu hizo mpya za kidiplomasia za Tillerson, zilikuja wiki mbili tangu Korea Kaskazini itangaze kufanikiwa kwa jaribio la kombora lake la masafa marefu la kisasa lenye uwezo wa kuipiga Marekani.

Hata hivyo, baada ya Tillerson kutoa tamko hilo, Ikulu ya Marekani baadaye ikatoa taarifa ya kutatanisha, ambayo imeacha maswali iwapo Trump aliidhinisha kile kilichozungumzwa na Tillerson.

Katika taarifa hiyo, Trump alisema Tillerson anapoteza muda wake kwa kujaribu kuishawishi Korea Kaskazini kuingia katika mazungumzo.

Kadhalika Ikulu ya Marekani imesema msimamo wa Trump haujabadilika kuhusu Korea Kaskazini na kwamba vitendo vinavyofanywa na nchi hiyo si vizuri kwa mtu yeyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles