25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MKAPA AMMWAGIA SIFA KAGAME

Na Arodia Peter-Kigali, Rwanda


RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amesema Rais wa Rwanda, Paul Kagame anastahili sifa ya pekee kwa kuivusha nchi hiyo kwa jamii na uchumi huku akizitaka nchi za Afrika kujifunza kutoka kwake.

Amesema licha ya changamoto ya vita iliyoikumba nchi hiyo miaka 30 iliyopita, bado imekuwa ni moja ya nchi zinazoendelea kukuza uchumi wake kwa kasi.

Kauli hiyo aliitoa juzi alipohutubia katika maadhimisho ya miaka 30 ya chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF).

Alisema Rwanda imepiga hatua kubwa ya maendeleo  na imekuwa ya kupigiwa mfano kwa nchi za Afrika.

Maadhimisho hayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha ajenda mpya ya mabadiliko ya jamii na uchumi Afrika ambayo yalihudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani wakiwamo wachumi na waandishi wa habari.

“Katika kiswahili kuna msemo usemao, ‘usione vyaelea vimeundwa’. Rais Kagame amefanya kazi kubwa kufikia haya maendeleo tunayoyaona leo ambako Rwanda ni nchi inayoendekea kwa kasi uchumi, jamii na utamaduni pia,” alisema Mkapa

Rais huyo mstaafu alisema nchi za Afrika kama zinataka maendeleo zijifunze kusikiliza wanaongoza na kuacha ubinafsi.

Alishauri viongozi wa Afrika kufanya mabadiliko ya dhati ya siasa na uchumi kwa kutoa vipaumbele kwa makundi ya vijana na wanawake katika uongozi.

Alitoa mfano kwa CCM ambacho alisema kimetenga nafasi maalumu za uwakilishi wa makundi hayo ndani ya Bunge.

“Makundi haya ni muhimu katika maendeleo ya sasa kwa sababu  yakiachwa nyuma nchi haiwezi kupiga hatua ya maendeleo,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa RPF, Ngarambe Francois alisema nchi hiyo imepiga hatua za haraka katika uchumi na jamii kutokana na wananchi wake kutambua na kuwa wazalendo wa kweli kwa taifa lao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles