30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ASKOFU NIWEMUGIZI ATOA WARAKA MZITO

Na NORA DAMIAN-DAR ES SAALM


SIKU chache baada ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge, Wilaya ya Ngara  mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61) kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na uraia wake, kiongozi huyo wa dini ametoa waraka unaohusu umuhimu wa Katiba mpya.

Katika waraka huo alisisitiza kuwa maoni yake kuhusu Katiba mpya  hayawakilishi msimamo wa Kanisa Katoliki bali  ni yake binafsi.

Askofu Niwemugizi ambaye juzi aliliambia MTANZANIA kuwa aliitwa mara mbili na Uhamiaji kuhojiwa, alisema ataendelea kuizungumzia Katiba mpya kwa sababu inagusa maisha yake na Kanisa analolitumia   na maisha ya watanzania kwa ujumla.

“Bado nitaendelea kuizungumzia Katiba kwa sababu inagusa maisha yangu na Kanisa   ninalotumikia, lakini pia inayagusa maisha ya raia wenzangu wote.

“Kwa vyovyote naheshimu tofauti zetu za kuwaza na kuona mambo, kwa sababu  ndivyo ilivyompendeza Mungu kutuumba, hatufanani tangu sura hadi kuwaza.

“Nilifurahi nilipopingwa, nikajua kuwa lengo limefanikiwa kuchokoza  tuanze tena kuzungumzia mchakato wa Katiba.

“Bado siogopi kukoromewa na sauti nzito, nikijua kuwa hata Yesu alikoromewa na wakuu!  Naamini hatimaye kitu kizuri kitazaliwa baada ya michango ya mawazo kwa lengo la kujenga.

“Mimi siamini kuwa Katiba mpya ilikuwa kipaumbele wakati ule tu na sasa siyo. Kwa hiyo kwa kweli si kwamba tunavumbua gurudumu jipya, bali ni kulifanya lile lililokwisha kuanza kuzunguka liendelee,”alisema askofu huyo.

Askofu Niwemugizi alisema hata   ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilibeba agenda hiyo kama jambo la kukamilisha katika   miaka mitano ijayo.

Alisema anaamini  watanzania wengi wanahitaji Katiba hivi sasa lakini yawezekana wale wenye jukumu la kuhakikisha inapatikana wana majukumu mengi.

Aliwashauri wenye majukumu hayo washughulikie haraka yale wanayoona yinafaa haraka zaidi kwanza kabla ya Katiba.

SOMA WARAKA WA ASKOFU  NIWEMUGIZI NENO KWA NENO KATIKA GAZETI HILI KESHO.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles