24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

IMF YAITAHADHARISHA TANZANIA

Na MWANDISHI WETU


SHIRIKA la Fedha Duniani (IMF) limesema idadi ya watu  nchini  inatarajia kuongezeka katika miongo miwili ijayo.

Limeishauri  Serikali   kujiandaa kwa kutengeneza mazingira mazuri ya ajira.

Hayo yalielezwa na ujumbe wa shirika hilo uliokuwa ukiongozwa na Mauricio Villafuerte, ambao umekuwapo nchini tangu Novemba 30 hadi Desemba 12  mwaka huu.

Lengo la ujumbe huo lilikuwa kupitia sera mbalimbali za uchumi na kuangalia mwenendo wa uchumi kabla ya kutoa ushauri kwa Serikali kufuatana na mpango unaojulikana kama Policy Support Instrument (PSI).

Taarifa iliyotolewa   baada ya kumaliza shughuli zake, ilisema   Tanzania bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika kutekeleza  malengo yake ya maendeleo.

Waliitaka Serikali kufanyia kazi changamoto hizo ikiwamo kuimarisha mazingira ya kufanya kazi kwa sekta binafsi.

“Wakati idadi ya watu ikitarajiwa kongezeka katika kipindi cha miaka 20 ijayo, kuandaa mazingira bora kwa ajili ya sekta binafsi kutengeneza ajira, ni jambo la kipaumbele.

“Kuboresha mazingira ya biashara, kuwa na sera zinazotabirika ambazo zinajali maoni kutoka sekta binafsi, maboresho kwenye sera za udhibiti  na kurudisha kodi kama VAT na nyinginezo kwa muda muafaka   na kulipa madeni ya ndani, ni baadhi ya mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema takwimu zilizotolewa na mamlaka za Tanzania mwanzoni mwa mwaka 2017, zinaonyesha ukuaji wa uchumi   wa aslimia 6.8.

Hata hivyo, taarifa hiyo iliitaka Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) kuangalia upya vyanzo   na utaratibu wake wa kuandaa takwimu zinazoeleza ukuaji wa uchumi……….

Kwa habari zaidi pata nakala yako ya MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles