23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Nkurunzinza ameweka picha mbaya katika soka’

pierreNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM
CHAMA cha Makocha wa Soka Nchini (Tafca) kimeeleza kuwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, ameuweka mchezo wa soka kwenye picha mbaya kutokana na kitendo chake cha kujiongezea muda wa kukaa madarakani.
Nkurunzinza amepitishwa na Chama chake cha CNDD-FDD kugombea kwenye uchaguzi ujao wa Burundi kwa muhula wa tatu Juni 26 mwaka huu, jambo ambalo limepingwa na kuleta machafuko nchini humo.
Juzi Meja Jenerali Godefroid Niyombare aliyaongoza majeshi ya nchi hiyo kumpindua Nkurunziza, ambaye alikuwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kikao cha marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati (EAC) kujadili mgogoro wa Burundi.
Katibu Mkuu wa Tafca, Michael Bundara, aliliambia MTANZANIA jana kuwa lazima Nkurunziza aruhusu demokrasia ndani ya nchi yake na kuachana na udikteta ambao anataka kuufanya kwa kujiongezea muda.
“Ametuweka kwenye picha mbaya sisi watu wa soka kutokana na kitendo chake hicho cha kujiongezea muda, kwani yeye alikuwa ni mwanamichezo mzuri, kocha pamoja na mwanasoka wa zamani wa Burundi.
“Sasa angalia machafuko yanayotokea na watu wake wanauawa kwa majeshi kulinda madaraka yake, hata huyu aliyefanya mapinduzi naye sijui kama atapenda kuachia madaraka, ameiweka kwenye hali mbaya nchi yake na pia yeye amejiweka pabaya kwani atakuwa akiishi maisha ya wasiwasi,” alisema.
Bundara aliongeza kuwa Nkurunziza alipaswa kufuata mfano wa mwanasoka wa zamani wa dunia, George Weah raia wa Liberia aliyekubali kushindwa kwenye uchaguzi wa nchi hiyo kwa awamu mbili tofauti (2005 na 2011) mbele ya mwanamama Ellen Johnson Sirleaf, bila mitafaruku yoyote.

Nkurunziza katika michezo
Nkurunziza ni mpenzi wa mchezo wa soka na baiskeli, alianza kucheza soka akiwa na umri wa miaka mitano alizichezea timu za sekondari na chuo kikuu.
Rais huyo alitumia ujuzi wake kwenye soka kufundisha wachezaji, aliwahi kuwa kocha wa timu ya Union Sporting inayoshiriki Ligi Kuu Burundi miaka ya 1990, wakati akiwa waziri katika Serikali ya nchi hiyo mwaka 2004 alianzisha kituo cha soka (Academy) kilichokuwa kikifundisha watoto takribani 600 wa Burundi.
Mbali ya kufanikiwa kujenga shule takribani 5,000, pia amejenga viwanja vya soka 10 kutokana na kuwa mkristo, Nkurunziza pia anaelezwa ya kuwa alikuwa mmoja ya waimbaji wa kwaya yake aliyeianzisha inayoitwa Hallelujah pamoja na timu yake ya soka inayoitwa Hallelujah FC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles