23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 11, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yazima ndoto za Msuva Sauzi

msuvaNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
NDOTO za mshambuliaji wa timu ya Yanga na mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Simon Msuva kucheza soka la kulipwa katika timu ya Bidvest Wits nchini Afrika Kusini zimefutika, baada ya uongozi wa Wanajangwani hao kumzuia mchezaji huyo kuondoka.
Habari za kuaminika kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo zililieleza MTANZANIA jana kuwa, maamuzi hayo yalitolewa katika kikao kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Chanzo hicho kilisema kuwa sababu ya uongozi kumzuia Msuva ni kutokana na dau la dola 100,000 sawa na milioni 200 za Kitanzania, ambazo Yanga wangekabidhiwa kama wangekubali kumtoa mchezaji huyo.
“Fedha ambazo Bidvest Wits wamesema watatoa ni ndogo sana ukilinganisha na gharama ambazo Yanga wamezitumia kwa Msuva tangu asajiliwe kutoka Moro United mwaka 2012, kwani zinajumuisha uhamisho wake na malipo yake binafsi ambazo ni ndogo sana, unadhani Yanga watabakiwa na kiasi gani,” kilisema chanzo hicho.
Mpasha habari huyo alisema sababu nyingine iliyofanya uongozi kugoma kumuuza mchezaji huyo ni kuwa ana mkataba ambao unamalizika mwakani.
Mchezaji huyo alirejea nchini hivi karibuni akitokea Afrika Kusini alipokwenda kufanya majaribio na kufuzu kuichezea timu hiyo.

Msuva angekuwa mchezaji wa pili wa Yanga kutimkia Afrika Kusini baada ya winga Mrisho Ngassa kutimkia huko.
Ngassa mapema wiki hii amesaini mkataba wa miaka minne kuchezea timu ya Free State Stars, akilipwa mara tatu ya mshahara aliokua analipwa Yanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles