25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NKAMIA ATAKA UCHAGUZI KILA BAADA YA MIAKA SABA

Na MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), anatarajia kuwasilisha muswada binafsi kulitaka Bunge liridhie marekebisho ya katiba itakayoruhusu Uchaguzi Mkuu uwe unafanyika baada ya miaka saba badala ya mitano ya sasa.

Nkamia alisema katika taarifa yake aliyoitoa jana, kwamba kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano ni gharama kubwa kwa nchi masikini kama Tanzania.

Katika hoja yake hiyo, Nkamia pia anataka Uchaguzi Mkuu uhusishe uchaguzi wa Serikali za Mitaa kupunguza gharama.

“Katika kipindi cha miaka mitano, nchi imekuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa miaka miwili kabla ya Uchaguzi Mkuu na hivyo kufanya gharama ya uchaguzi kuwa kubwa.

“Hatua hiyo inasababisha Serikali badala ya kushughulikia kero za wananchi, imekuwa ikishughulika kutafuta fedha za maandalizi ya uchaguzi kwa muda mrefu,” alisema Nkamia.

Alisema pamoja na kuuarifu uongozi wa chama chake ndani ya Bunge, anatarajia kumwandikia Spika kuhusu kusudio hilo.

Alitoa mfano nchi ya Rwanda ambayo alisema ni ndogo, lakini inafanya uchaguzi kila baada ya miaka saba na ndiyo miongoni mwa nchi za Afrika zinazopiga hatua katika maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles