22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

‘Ningefanyaje’ yamfungia mwaka Ben Pol

benNA BADI MCHOMOLO

MKALI wa muziki wa RnB nchini, Benard Paul ‘Ben Pol’, anaumaliza mwaka kwa kuachia video ya Ningefanyaje ambayo amemshirikisha msanii kutoka nchini Kenya, Aviril Nyambura.

Video hiyo tayari imeachiwa jana katika vituo mbalimbali vya runinga hapa nchini, huku ikiwa imeandaliwa na mtayarishaji Mswaki.

Ben Pol amesema vipande vya video hiyo vimefanyika mjini Pretoria, nchini Afrika Kusini chini ya mwongozaji, Justin Campos, akiwa na kampuni yake ya Gorilla Films.

Msanii huyo amesema wimbo huo unaelezea ukweli kuhusu rafiki yake wa karibu baada ya kutendwa na mpenzi wake na kuamua kuendelea na mambo yake.

“Hii ni video yangu ya mwisho kwa mwaka huu, ninaamini nitakuwa naumaliza mwaka vizuri, kinachobaki ni kumuomba Mungu tuuone mwaka mpya na kazi mpya,” alisema Ben Pol.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles