24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Azam: kila mechi Kwetu ni fainali

azam-1NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Azam FC umesema kwamba kuelekea kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kila mechi watakayocheza itakuwa kama fainali.

Klabu hiyo ipo nafasi ya pili kwenye ligi hiyo ikiwa na tofauti ya pointi moja nyuma ya klabu ya Yanga, ambayo ina pointi 30 baada ya kucheza michezo 12.

Akizungumza na MTANZANIA, Msemaji wa klabu hiyo, Jafari Iddi, alisema kwamba wapo katika maandalizi ya mechi yao dhidi ya Kagera Sugar Jumapili hii.

“Kwa sasa timu inajiandaa kuingia kambini kwa ajili ya mechi ya Kagera Sugar ambayo itafanyika Jumapili, hata hivyo hadi sasa tuna majeruhi wawili mlinda mlango, Aishi Manula pamoja na Agrey Morris,” alisema Iddi.

Akizungumzia ushindani uliopo dhidi ya kinara wa msimamo huo ambao ni klabu ya Yanga, alisema hawana haja ya kuwajadili na kudai kwamba lengo lao ni kuwa mabingwa wa ligi hiyo.

“Leo tunaingia kambini ili kujiandaa na mechi ya Jumapili kwa kuwa Kagera si klabu ya kuibeza ndiyo maana tunatakiwa kufanya mazoezi ya kutosha,” alisema Iddi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles