30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Pluijm atoa angalizo kwa wachezaji

pluijmNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans Van der Pluijm, amesema kuwa hafikirii kama kikosi chake kitatoka kwenye nafasi tatu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo ametoa angalizo kwa kila mchezaji kuhakikisha anaendana na kasi yake.

Timu hiyo juzi ilifanikiwa kuongoza ligi, baada ya kushinda mabao 4-0 dhidi ya Stand United na kufanikiwa kufikisha jumla ya pointi 30.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema tayari ameshapiga hesabu za mbali na kuamua kutoa angalizo hilo kwa wachezaji wake.

Pluijm alisema kikosi chake kinachoongoza ligi kwa sasa, kitaendelea kubaki katika nafasi hizo za juu kutokana na malengo waliyojiwekea.

“Sifikirii kuona kikosi changu kikishuka nafasi za chini kwenye msimamo, unajua hivi sasa tunapambana kuendeleza matokeo bora tunayoyapata sasa kama kuna mchezaji ambaye hataendana na kasi ninayotaka tutamwacha nyuma.

“Wakati ligi imesimama nilikuwa naendelea kuandaa programu zangu nitakazotumia kuisaidia timu yangu kubakisha heshima ile tuliyoanza nayo msimu huu, nashukuru hilo limefanikiwa na tutaendeleza mapambano hadi ushindi utakapokuwa mikononi mwetu,” alisema Pluijm.

Yanga inatarajiwa kuvaana na Mbeya City katika mchezo ujao uliopangwa kufanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles