Shamsa amvulia kofia Irene Uwoya

0
1519

Shamsa_Ford_02NA THERESIA GASPER

MSANII wa filamu nchini, Shamsa Ford, amesema katika wasanii ambao anawakubali kutokana na ubora wa kazi zao mmojawapo ni Irene Uwoya.

Shamsa alisema msanii huyo anajua nini anachofanya na anapenda kupeana ushauri na kushirikiana katika mambo mbalimbali na wenzake.

Shamsa aliyasema hayo alipokuwa akimkabidhi zawadi Irene katika sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake Sinza, Dar es Salaam.

“Tabia yangu na ya Irene inaendana kwani tumekuwa tukifanya vitu kwa ushirikiano, nampenda sana na tumekuwa tukishauriana vitu vya msingi kwani ni yeye aliyenishauri na mimi nizae,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here