MSANII wa hip hop, Nickson John ‘Nick M’bishi’, amesema yupo tayari kushirikiana na msanii yeyote ndani na nje ya nchi kama wakimhitaji.
“Wasanii tumekuwa watu wa kubaniana ila mimi nipo tayari kushirikiana na msanii yeyote atakayenitaka ili kuufikisha muziki wetu wa hip hop mbali,” alisema Nick M’bishi.