24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

NGUVU ZA KIUME, KUKOSA FURAHA KWAMTESA MBUNGE

Katika hali inayoonyesha kukithiri kwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, serikali imetakiwa kuwasaidia wananchi wake ambao wengi wana tatizo hilo na kuelezea kwa nini imekuwa nchi ya mwisho kwa watu wake kukosa furaha.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Septemba 6, Mbunge wa Konde, Khatibu Haji (CUF), amesema tatizo hilo pia limekuwa likiwasumbua hata baadhi ya wabunge kwani wamempelekea ‘Memo’ wakielezea shida zao juu ya tatizo hilo ambapo amesema hivi sasa kuna utitiri wa matangazo ya biashara ya dawa za kuongeza nguvu za kiume hatua inayoashiria ukubwa wa jambo hilo.

“Je Wizara inachukua hatua gani kwa sababu utumiaji wa madawa kiholela unazidisha matatizo mbalimbali na kuna kabila moja kila unapokutana naye njiani anauza dawa hizo, kwa hiyo naomba wizara itoe tahadhari na kuchukua hatua juu ya madawa ambayo yanasambaa.

“Mheshimiwa Naibu  Spika tendo la raha linahitaji furaha kuna taasisi imeeleza kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi 10 duniani ambayo wananchi wake wamepoteza furaha, sasa ni miaka 50 ya uhuru, je kwanini nchi yetu  iko katika nafasi ya mwisho duniani kwa kupoteza furaha mmekosea wapi? amehoji mbunge huyo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala amekiri Watanzania wengi kusumbuliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

“Kwanza nianze kwa kukubaliana na Khatibu Said Haji, kwamba tendo la raha linahitaji furaha na ni kwa msingi huo changamoto zinazowapata wanaume wa kisasa kwenye tendo hili zinatokana kwa kiasi kikubwa na kukosa furaha, msongo wa mawazo na ongezeko kubwa la magonjwa ambayo si ya kuambukiza.

“Hizi ni sababu kubwa kuliko zote kwamba ukiwa na msongo na uchovu kwa hakika huwezi kuwa na ile hamasa ya kushiriki tendo la ndoa ipasavyo na hii ni sababu mojawapo na ndio maana nashangaa watu ambao wanahangaika sana kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume, hiyo ni changamoto ya kimwili lazima uwe na afya njema, uwe huna magonjwa lakini pia hutumii madawa kwa muda mrefu lakini pia uwe umetulia, uwe na amani katika moyo wako na hiyo huwezi  kupata raha kama huna furaha,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles