24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Nguo zenye viyoyozi zaja

p3900147-1200x800

Na Jonas Mushi,

WATAFITI nchini Marekani (ARPA-E) wamefadhiliwa na idara ya nishati nchini humo kutengeneza nguo ambazo zinaweza kubadilisha hali ya joto kuendana na mazingira na mwili wa mvaaji.

Lengo ya kuwapo kwa nguo hizo licha ya kuwapo kwa viyoyozi ni kwamba itaongeza wigo wa mtu kuwa katika hali nzuri akiwa katika mazingira mbalimbali na si ndani ya nyumba au gari kama ilivyo sasa.

Nishati ya joto inaweza kusafiri kwa njia kuu tatu; kwanza ni kwa njia ya kitu kigumu (conduction) ambapo atomu za kitu husafirisha nishati hiyo kutoka kwa atomu moja kwenda nyingine; njia ya hewa (Convection) ambapo atomu zenye nishati kubwa husambaa hewani.

Njia nyingine ni ya mionzi (Radiation) ambapo nishati ya joto kusambaa kama mawimbi sumaku (electromagnetic waves). Nguo inaweza kudhibiti joto kwa kubadili kiasi cha mionzi kinachoruhusiwa kutoka mwilini au mzunguko wa hewa kirahisi.

Timu ya Alon Gorodetsky ya Chuo Kikuu cha California,  inasema inalenga kudhibiti joto la mionzi kwa vitu ambavyo vina sifa ya kudhibiti ikiwamo ‘squid’ na ‘cephalopods’

‘Squid’ inaweza kudhibiti mionzi kwa namna inavyoakisi miale ya mwanga kwa kutumia protini iliyopo kwenye ngozi. Timu hiyo inaangalia namna ya kutumia fursa hiyo ya miale ambayo huwa na joto.

“Tunataka tutumie fursa ya sifa za vitu vinavyodhibiti upoteaji wa joto wa kitu,” inasema timu hiyo japo hajaweza kuonyesha namna timu hiyo itakavyotumia cephalopod kama kidhibiti mionzi.

Timu yake inashirikiana na kampuni ya Under Armour ya nchini humo ambayo hutengeneza matabaka ya chini ya nguo za michezo.

Mfumo wa mirija

Timu ya Jintu Fan ya Chuo Kikuu cha Cornell huko Ithaca, New York, inatumia njia tofauti kwa kudhibiti mzunguko wa hewa ya joto na baridi kupitia mtandao wa mirija midogo iliyowekwa kwenye vesti.

“Zaidi ya hapo unaweza kuivaa mahali  popote unapotaka,” anasema Fan.

Vihisijoto vya vesti husimamia ngozi kwa kuingiza ndani hewa ya joto au baridi kadiri itakavyotakiwa.

“Ni kama mfumo wa kiyoyozi kidogo ambacho kipo mwilini mwako.” anasema Fan.

Nguo zinazodhibiti joto la mwili si ngeni hadi sasa hutumika kwenye nguo kubwa zinazotumiwa na wanajeshi, wanajimu, watu wa huduma za dharura au katika maabara za majaribio.

Wanajimu huvaa makoti ya kudhibiti joto wanapokuwa ndani ya vifaa vya kusafiria angani ambavyo hutumia kimiminika kuondoa joto na makoti hayo ni mazito.

ARPA-E wamewekeza dola za kimarekani milioni 30 kutengeneza mfumo ambao ni mzuri wa kuvaa katika maisha ya kawaida ya kila siku.

Watafiti hao wanasema wanataka nguo hizi kila mtu aweze kuwa nazo kama anavyokuwa na nguo zingine za kawaida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles