Vyuo vikuu 10 vinavyovutia wanafunzi wa kimataifa

florida university
Chuo Kikuu cha Florida, Marekani.

 

NA FARAJA MASINDE,

TAKWIMU zinaonyesha kuwa katika kila chuo kimoja nchini Marekani kina asilimia 19 ya wanafunzi wa kigeni wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao hapo.

Ni kweli kuwa kila siku idadi ya wanafunzi wa kigeni inaendelea kuongezeka kwenye vyuo mbalimbali duniani hususan vyuo vya Marekani.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanafunzi wa kigeni katika vyuo vya Marekani inazidi kuongezeka ambapo katika mwaka wa masomo wa 2014/2015 iliongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Ripoti zinasema kuwa jumla ya wanafunzi 974,926 kutoka kote duniani walikuwa wakisoma kwenye vyuo vya Marekani katika mwaka wa masomo wa 2014/15.

Huku wanafunzi kutoka Latini Amerika na Visiwa vya Caribiani wakiwakilisha kundi kubwa la wanafunzi wa kigeni waliokuwa wakisoma nchini humo ambao ni asilimia 19.

Vyuo hivyo 10 ni vile ambavyo vimekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa kimataifa waliosoma hapo ama wale ambao bado wapo masomoni, ambapo kwa wastani ni asilimia 22 ya wanafunzi kutoka kote ulimwenguni walisoma kwenye vyuo hivyo kwa mwaka 2014.

Ambapo kwa mwaka jana asilimia moja ya wanafunzi iliongezeka kwa mujibu wa takwimu za taarifa za Marekani zilizoonyesha vyuo bora 266 na kila chuo kilidahili wastani wa wanafunzi wapatao 7,216 kwa mwaka.

Chuo cha Tekinolojia cha Florida kinaonekana kuwa na kiwango kikubwa cha wanafunzi wa kigeni ambapo kwa mwaka 2014 kilikuwa na asilimia 32.9 ya wanafunzi wa kigeni na hivyo kuifanya taasisi ya vyuo vikuu nchini Marekani kuwagharamia wanafunzi hao kusoma bure mafunzo ya udaktari.

Hata hivyo, Chuo Kikuu cha Central Florida ndicho kinachoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa kigeni kwa mujibu wa baraza la elimu ya juu la Marekani.

Hapa chini ni orodha ya vyuo hivyo na kiwango cha wanafunzi wa kigeni kwenye mabano pamoja na asilimia, vyuo hivi vimekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofika kuchukua shahada kwa kipindi cha mwaka wa masomo wa 2014/15 nchini Marekani.

Chuo cha kwanza ni Florida Institute of Technology (wanafunzi 3,636 sawa na asilimia 32.9 huku kikishika nafasi ya 161 kwa ubora Vyuo Marekani), New School (NY) (wanafunzi 6,695 sawa na asilimia 31.7 kikiwa ni cha 127 kwa ubora), Taasisi ya Tekinolojia ya Illinois (wanafunzi 3,099 sawa na asilimia 29.8 nafasi ya 108 kwa Marekani).

Vyuo vingine ni Tulsa (OK) (3,473 sawa na asilimia 26.7 kikiwa katika nafasi ya 86 kwenye ubora), Chuo Kikuu cha Lynn (FL) (1,976 sawa na asilimia 23 huku kikiwa hakiko kwenye orodha ya vyuo bora Marekani), Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon (PA) (6,309 (20.9%) nafasi ya 23).

Vingine ni Chuo Kikuu cha California—San Diego (24,810(19.9) nafasi ya 39), Chuo Kikuu cha Andrews (MI) (1,805 (19.6%) nafasi 175), Chuo Kikuu cha Northeastern (MA) (13,510 (19.1%) nafasi ya 47) na nafasi ya 10 ni Chuo Kikuu cha San Francisco (6,845 (19%) nafasi ya 1080.

Vyuo vya Marekani kwa miaka ya hivi karibuni vimekuwa vikitajwa kufanya vizuri kiwango ambacho kimefanya ving’are mbele ya vyuo vya Uingereza kutokana na mataifa haya mawili kuwa na ushindani wa kielimu.

Inaelezwa kuwa uwapo wa mazingira rafiki pamoja na miundombinu thabithi kwa wanafunzi ndiyo imekuwa siri ya wanafunzi wengi duniani kukimbilia nchini humo kuendeleza taaluma zao jambo ambalo linapaswa kuigwa na serikali za Afrika kwa kuwa karibu na vyuo vya ndani ili kuwa kivutio na kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here