29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

NEWCASTLE UNITED, TOTTENHAM ZAPIGWA

LONDON, ENGLAND

LIGI Kuu nchini England iliendelea jana kwenye viwanja viwili, huku mchezo wa awali ukiwakutanisha Newcastle United na kuchezea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Huddersfield Town.

Hicho ni kichapo cha pili kwa Newcastle United katika mchezo wa pili wa ligi kuu, baada ya mchezo wa ufunguzi kupokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Tottenham.

Mchezo wa jana dakika 45 za kipindi cha kwanza, Newcastle walionekana kutafuta bao, lakini hadi wanakwenda mapumziko hawakupata bao.

Baada ya kipindi cha pili kuanza, wenyeji wa mchezo huo Huddersfield Town walipambana kutafuta bao la mapema na wakafanikiwa katika dakika ya 50 lililofungwa na nyota wao Aaron Mooy.

Bao hilo liliwapa nguvu na jeuri wenyeji hao na kuamua kuweka ukuta, huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Newcastle United walijaribu kulizonga lango la wapinzani wao mara kwa mara, lakini ukuta wa Huddersfield Town ulizidi kuwa imara hadi dakika 90 zinamalizika.

Huddersfield Town imeonekana kuja juu baada ya kupanda daraja msimu huu, hadi sasa imefanikiwa kuwa na pointi sita baada ya kucheza michezo miwili na kushinda yote.

Mchezo mwingine ambao ulipigwa jana na kuteka hisia za mashabiki wengi ulimwenguni ni kati ya Tottenham dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Chelsea.

Chelsea walishuka dimbani huku wakiwa na hasira ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Burnley kwa mabao 3-2.

Baada ya kupoteza mchezo huo, kocha wao, Antonio Conte aliwaambia wachezaji wake wahakikishe wanashinda mchezo wao wa pili ambao ni huo wa jana na walifanikiwa kushinda mabao 2-1.

Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao la kwanza katika dakika ya 24 lililofungwa na nyota wake Marcos Alonso, lakini wapinzani wao walikuwa wanakuja kwa kasi kutafuta bao la kusawazisha.

Totteham walipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 82 baada ya nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi kujifunga wakati anaokoa mpira wa adhabu.

Dakika ya 88, Alonso alipeleka kilio kwa mashabiki wa Tottenham baada ya kupachika bao la pili.

@@@@@@@@@@@

 

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles