22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

NEC YAMNG’ANG’ANIA MGOMBEA CHADEMA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


 

MKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhan Kailima, amesema licha ya mgombea wa ubunge David Djumbe wa Singida Kaskazini kujitoa katika kinyang’anyiro hicho, bado wanamtambua ni mgombea halali.

Amesema mgombea huyo aliwasilisha barua ya kujitoa juzi, lakini NEC ilimgomea kwa kuwa barua hiyo badala ya kusainiwa na hakimu imesainiwa na wakili.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kailima alisema kuwa mgombea huyo amekidhi vigezo kwa mujibu wa sheria.

“Ili kuthibitisha kuwa David Djumbe ni mgombea halali wa Chadema, Desemba 19, mwaka huu (juzi), aliwasilisha  barua ya kutaka kujitoa katika kinyang’anyiro hicho, lakini tume ilimkatalia kwa kuwa barua aliyowasilisha ilisainiwa na wakili badala ya hakimu,” alisema Kailima.

Pamoja na ufafanuzi huo wa Kailima, mgombea huyo pamoja na Chadema bado wamesisitiza kuwa hawatoshiriki uchaguzi huo na barua waliyowasilisha imefuata utaratibu wote unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Wagombea wengine walioteuliwa ni Omari Sombi (AFP), Dalphina Patrick Mlewa (CUF), Monko Justine Joseph  (CCM),  Aloyce Mohamedi Nduguta (ADA TADEA) na Mchungaji Yohana Samuel Labisu (CCK).

“David Djumbe aliwasilisha barua ya utambulisho wa mgombea kutoka Chadema, iliyosainiwa na Katibu wa Chadema Wilaya ya Singida Vijijini, Ndugu Amani Mloya, alipewa fomu ya uteuzi namba 8B ambapo kipengele C kilijazwa na Katibu wa Chadema Wilaya kuonyesha kuwa amedhaminiwa na chama na pia amejaza fomu namba 10 kukiri kufuata na kutii maadili ya uchaguzi mbele ya msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo,” alisema Kailima.

Mbali na hilo, alisema kuwa Chadema waliwasilisha ratiba ya mapendekezo ya kampeni kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo sambamba na kumteua Shaban Lyimo kuwa mjumbe wa Kamati ya Maadili ambapo juzi alishiriki katika  kikao na kupitia ratiba za kampeni za vyama vya siasa vilivyosimamisha wagombea katika jimbo hilo.

Kailima amewataka viongozi wa Chadema kusoma vizuri na kufuata sheria za uchaguzi kwani ni haki ya mgombea  kujitoa na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 Kifungu cha 48 (1) na (2) kinaelekeza taratibu za kujitoa mgombea  ni kuandika barua binafsi ya kujitoa na kuwasilisha hati ya kiapo cha kujitoa iliyosainiwa na hakimu.

Kuhusu sababu zinazotajwa na Chadema kujiengua katika kinyang’anyiro hicho kuwa ni hofu juu ya usalama wao, Kailima alisema jukumu la kusimamia usalama lipo chini ya Jeshi la Polisi na si NEC na kuwa madai hayo yawasilishwe Jeshi la Polisi

Alisema zipo sababu za kisheria zinazosababisha kuahirishwa uchaguzi, lakini si kwa sababu chama kimoja cha siasa kimeamua kujitoa……

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles