23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ndoto za Taifa Stars kwenda Qatar 2022 zimezima hivi

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefungwa mabao 3-0 na DR Congo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kuifanya safari ya Tanzania kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022 kuishia hapa.

Mabao ya DR Congo yamefungwa na Gael Kakuta dakika ya saba, Nathan Idumba dakika ya 66 na Ben Malonga dakika ya 85.

Ndoto za Tanzania kufuzu michuano hiyo, zimepotea hasa baada ya Benin kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Madagasca na kufikisha pointi 10 zinazowafanya kuwa vinara wa kundi J.

Kwa matokeo hayo kulingana na msimamo wa kundi ulivyo, Benin na DR Congo ndizo zenye nafasi ya kwenda hatua ya mtoano baada ya mchezo wao wa mwisho zitakapokutana Novemba 14, 202, DR Congo wakiwa nyumbani.

Taifa Stars itacheza na Madagasca Novemba 14, 2021 ugenini kukamilisha ratiba ambapo kwa sasa ipo nafasi ya tatu na pointi saba.

DR Congo nafasi ya pili na alama nane, wakati Madagasca ya mwisho katika kundi na pointi tatu.

Aidha matokeo ya Uganda kutoka sare ya 1-1 na Kenya kumeufanya Ukanda wa CECAFA kukosa mwakili katika kombe la Dunia mwakani kwani timu zote zitacheza mechi za mwisho kukamilisha ratiba.

Uganda ipo kundi E na pointi tisa, Mali ambayo imefanikiwa kusonga mbele baada ya kuifunga Rwanda mabao 3-0 na kufikisha pointi 13.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles