24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Coca Cola yakabidhi soko la wamachinga Kigogo

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Coca Cola imekabidhi soko la wafanyabiashara wadogo 100  â€˜â€™wamachinga’ kwa Serikali  walilojenga eneo la  Kigogo Dampo,  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kufungua soko hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Mmejuwa kutufariji wakati wa shida, tukiwa tupo kwenye changamoto ya machinga ndio mmeweza kutufikiria na kutukabidhi soko, sisi kama serikali tutahakikisha tunalitanua na kuwa kubwa zaidi ili kuchukua wafanyabiashara wengi.

” Tutahakikisha hata magari yanakuja na kuleta watu waweze kununua vitu kwa wafanyabiashara watakaokuwa humu,” amesema Makalla.

Aidha amewashukuru kwa kuwa wamekuwa ni watu wanao wakimbilia na kuwasaidia katika kila changamoto, kwani waliweza kujenga vibanda Coco beach na sasa wamejenga soko Kigogo.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Unguu Sulay, amesema kuwa waliona ni vizuri kuweza kujenga soko ili kurahisisha wakazi wa Kigogo na maeneo ya karibu kupata mahitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles