26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ndoa za mashoga Stop

traditional-gay-marriageNA ESTHER MNYIKA,DAR ES SALAAM

TANZANIA  imeigomea Umoja wa Mataifa  (UN) kuhusu ndoa ya jinsia moja, katika mapendekezo   ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu.

Kaimu Mkurugenzi  wa Katiba  na Sheria na Haki za Binadamu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Alecia Mbuya  amesema hiyo ni kutokana  na mfumo wa nchi wa   sheria  sera, imani za dini, utamaduni, mila na desturi za nchi.

Akizungumza   Dar es Salaam jana alisema   mapendekezo  227 yaliyotolewa   na nchi wanachama wa UN ili Tanzania iyatekeleze.

Mbuya alisema mapendekezo hayo  yamejikita  katika  majukumu ya kimataifa    kwenye mikataba  mbalimbali ambayo Tanzania imeridhia.

Baadhi ya mikataba hiyo ni   masuala ya  katiba na  sheria,  haki za binadamu na masuala ya watu wenye ulemavu, alisema .

“Baada ya kupitia mapendekezo hayo Tanzania ilikubali kutekeleza mapendekezo 130 ambayo tuliyaona hayakinzani na katiba, sheria na sera zetu za nchi au yanahusu masuala ambayo tayari yapo kwenye hatua za utekelezaji,”alisema Mbuya.

Alisema Tanzania ilikataa kutekeleza mapendekezo 72 ambayo hayaendani na mfumo wa nchi wa  sheria ,sera, imani za dini ,utamaduni, mila na desturi.

Baadhi ya mapendekezo ambayo Tanzaninia ilikataa kutekeleza  ni   kufutwa  adhabu ya kifo, ndoa ya jinsia moja, masuala ya ubakaji ndani ya ndoa,  na kuridhia  mikataba ambayo haiendani na sheria za nchi, alisema.

Alisema  mapendekezo 25 hayakutolewa uamuzi na yaliahirishwa kwa kuwa yanahitaji kupata mwongozo kutoka kwenye vyombo vya uamuzi wa  sera au yanahitaji fedha kutumika na mapenekezo mengine ambayo yapo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

“Kwa muktadha huo, serikali itajitaidi kuyatekeleza mapendekezo ambayo imeyakubali kwa kushirikiana na wadau wote nchini.

“Tanzania inatakiwa kuwasilisha majibu ya mapendekezo  yaliyoahairishwa kabla ya kikao cha 33 cha Baraza la Haki za Binadanu kilichopangwa kufanyika Septemba mwaka huu,”alisema.

Alisema ofisi ya AG inakabiliwa na changamoto nbalimbali ikiwamo kushindwa kutekeleza majukumu muhimu ya ushirikiano wa  kanda na kimataifa kutokana na uwezo mdogo wa  fedha unaosababisha ushiriki mdogo wa shughuli hizo.

Alitaja changamoto nyingine kuwa   ofisi  haijaiwakilisha serikali kwenye majukwaa ya  kanda na kimataifa tangu mwaka 2014 na kuchelewesha  kuwasilisha taarifa za nchi za haki za binadamu  kutokana na ufinyu usiokidhi mahitaji ya ongezeko la majukumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles