27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

NDEGE YA MAKAMU WA RAIS AFGHANISTAN YAZUIWA KUTUA

KABUL, AFGHANISTAN

NDEGE iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa Afghanistan, Abdul Rashid Dostun ilizuiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Mazar-e Sharrif nchini hapa juzi.

Msemaji wake alisema Jenerali Dostun alikuwa amesafiri kwenda Uturuki Mei mwaka huu kwa ajili ya matibabu ya afya yake.

“Haijulikani ni nani aliyekataza kutua kwa ndege hiyo. Lakini Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan anasemekana kusema kuwa kurudi kwake hakukupangwa na serikali,” lilidokeza Shirika la Habari la Reuters mapema jana.

Kuna madai kuwa Dostun alikuwa amewaagiza watu wake kumteka nyara, kumpiga na hata kumbaka mpinzani wake wa kisiasa, Ahmad Eshchi ambaye awali alikuwa mshirika wake.

Hata hivyo Jenerali huyu amepinga madai hayo.

Jumatatu usiku ya wiki hii, Gavana mwenye nguvu wa Kaskazini mwa Mkoa wa Balkh Atta Mohammad Noor, alikuwa ameenda kumpokea mshirika wake huyo wa kisiasa kwenye Uwanja wa Ndege wa Mazar-e Sharrif.

Imeripotiwa kwamba zaidi ya watu 1000 waliandamana na gavana huyo kumpokea mpiganaji huyo wa zamani katika mpaka huo ambao uko karibu na mkoa wa nyumbani wa Jowzjan.

“Wafuasi wa Jenerali Dostun walikuwa na mabango yenye ujumbe ‘karibu nyumbani kiongozi wetu’, liliongeza Reuters.

Ripoti za awali zilidai majeshi ya Ujerumani yalikuwa nyuma ya hatua hiyo, lakini jeshi la Umoja wa Kujihami la Nato lilikana likisema maamuzi hayo yako ndani ya mamlaka za Afghanistan.

Chanzo cha habari  karibu na Rais Ghani kilisema uamuzi wa Dostun kurudi bila kuwasiliana na mamlaka za Kabul ulitiliwa shaka.

“Tulimtaka kwanza aje Kabul kwa sababu kuna masuala ya utatuzi kwanza. Hakuna vikwazo vya kisheria vinavyomkabili lakini anatakiwa afuate njia nzuri,” kilisema.

Hivi karibuni Jenerali Dostum, Atta Mohammad na kiongozi mwingine mwenye nguvu wa kikabila Mohammad Mohaqeq, waliunda kundi la upinzani linalotaka mageuzi makubwa ya kisiasa ikiwamo kupunguza mamlaka za rais.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles