BROWN: KARRUECHE ANANUFAIKA NA JINA LANGU NEW YORK, MAREKANI

0
458

STAA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, amefunguka na kusema kwamba mpenzi wake wa zamani, Karrueche Tran, anatumia jina la msimu huu kujiingizia kipato.

Mwezi uliopita mrembo huyo alienda mahakamani na kutoa taarifa kwamba bado anapata vitisho kutoka kwa msanii huyo, hivyo anatakiwa apewe ulinzi.

Kitendo hicho Brown kilimsikitisha sana na kusema kwamba kwa sasa yupo kimya kutokana na kuwaandalia mashabiki wake vitu vizuri na si kufuatilia wanawake.

“Nimekuwa mbali na Karrueche kwa muda mrefu, lakini nashangaa kuona bado jina langu analitumia katika mambo yake, ninaamini anakuwa anaingiza fedha kutokana na kulitumia jina langu kwa namna mbalimbali, siwezi kuzungumzia habari za wanawake kwa sasa kwa kuwa naandaa kazi bora kwa mashabiki wangu,” alisema Brown.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here