27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ndayiragije aitangazia silaha Sudan, Manula nje

Zainab Iddy, Dar es salaam

KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije ameita kikosi cha wachezaji 25 kujiwinda na mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Cameroon.

Stars inarajia kuanzia nyumbani dhidi ya Sudan, mechi itakayochezwa Jumapili ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika kikosi hicho, Ndayiragije ameendelea kutomjumuisha kipa wa muda mrefu katika kikosi hicho, Aishi Manula, huku akimtema Beno Kakolanya na Shomari Kapombe waliocheza dhidi ya Burundi kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022.


Kwa ujumla kikosi cha Taifa Stars kilichotajwa jana na Mrundi huyo ni kama ifuatavyo- Makipa; Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga SC) na Said Kipao (Kagera Sugar).
Mabeki; Haruna Shamte (Simba), Boniphace Maganga (KMC), Gardiel Michael (Simba SC), Mohammed Hussein (Simba), Kelvin Yondani, Erasto Nyoni (Simba), Iddy Mobi (Polisi Tanzania), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union).
Viungo; Jonas Mkude (Simba SC), Baraka Majogoro (Polisi Tanzania), Mohammed Issa ‘Banka’ (Yanga SC), Mudathir Yahya (Azam FC), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Frank Domayo (Azam FC), Muzamil Yassin (Simba SC), Abdulaziz Makame (Yanga SC), Hassan Dilunga (Simba SC) na Feisal Salum (Yanga SC).  


Washambuliaji; Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC), Miraj Athumani ‘Madenge’ (Simba SC), Shaaban Iddi Chilunda (Azam FC) na Ayoub Lyanga (Coastal Union).

Taifa Stars watarudiana na Sudan Oktoba 18 mjini Kampala nchini Uganda na mchezo huo umehamia huko kutokana na machafuko yaliopo nchini Sudan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles