Waziri atoa wiki tatu kituo cha afya kuanza kutoa huduma

0
560

Amina Omari, Pangani

Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Tamisemi), Suleiman Jaffo ametoa wiki tatu kwa Halimashauri ya Wilaya ya Pangani kuhakikisha kituo cha afya cha Mkalamo kinaanza kutoa huduma kwa wananchi.

Agizo hilo amelitoa leo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo hicho kilichopo wilayani humo.

Amesema kuwa mradi huo ulikuwa ukamilike toka mwishoni mwa mwezi uliopita hivyo ucheleweshaji wake unawanyima fursa wananchi ya kupata huduma karibu na maeneo yao.

“Nakuagiza mganga mkuu wa mkoa Dk Jonathan Budenu hakikisha unaleta watumishi hapa na ifikapo Oktoba 10, kituo kiwe kimeanza kazi,” amesema Waziri Jaffo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah amesema kuwa uwepo wa kituo hicho utawasaidia wananchi kupunguza umbali mrefu wa kufuata huduma.

“Wanawake na Watoto ndio walikuwa wahanga wakubwa kwani walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 40 kufuata huduma ya afya Pangani mjini,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here