29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

NDALICHAKO MGENI RASMI MAONYESHO YA SAYANSI


Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya kazi za wanasayansi chipukizi yatakayofanyika wiki ijayo, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam  jana, Mwanzilishi Mwenza wa Taasisi ya Wana sayansi Chipukizi (YST), Dk.Gosbeth Kamugisha alisema maonyesho hayo yatawakutanisha wagunduzi na watafiti kutoka  shule za sekondari nchini.

Alisema maonyesho yataakisi kazi za mwaka mzima, zilizokuwa zikisimamiwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na walimu 100 wa shule hizo ambazo zitajikita katika kutatua changamoto za kijamii, uchumi, afya, mazingira.

“Nawakaribisha wananchi wafike kujionea kazi zinazofanywa na wanasayansi chipukizi kwa siku mbili kuanzia asubuhi hadi saa 6.30 mchana,” alisema Dk.Kamugisha.

Alisema kutakuwa na majaji 50 kutoka vyuo vikuu, mashirika ya jamii, taasisi za sayansi na teknolojia ambapo watazikagua kazi zote zitakazooneshwa.

Kwa upande wa wadhamini wa maonyesho hayo, Karimjee Jivanjee Foundation(KJF), wameahidi kutoa udhamini wa masomo ya chuo kikuu kwa wanafunzi ambao kazi zao zitashinda.

Meneja wa KJF, Devotha Rubama alisema wana wasaidia chipukizi  ili watimize ndoto zao na kuisaidia jamii kuondokana na changamoto za afya, kijamii,uchumi na mazingira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles