27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

GEREZA LA KWITANGA KUZALISHA MICHIKICHI


Na Mwandishi Wetu, Kigoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Serikali imeliteua Gereza la Kwitanga lililopo wilayani Kigoma kuwa kituo kikuu cha uzalishaji wa zao la michikichi nchini.

Hivyo ameuagiza uongozi wa gereza hilo waongeze nguvu katika uzalishaji wa michikichi kwa kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha michikichi na kupanda miche mipya ya michikichi na kukata ya zamani.

Waziri Mkuu ameyasema jana, wakati alipotembelea gereza hilo akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma.

Alisema Serikali imedhamiria kwa dhati kufufua kilimo cha zao hilo mkoani Kigoma, hivyo kila mwananchi lazima awe na shamba la michikichi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimwagiza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, Sabas Matolo kuhakikisha  gereza hilo,linawezeshwa kwa kuwa na zana bora na za kisasa za kilimo yakiwemo matrekta na vifaa vya kuvunia ili waweze kuongeza uzalishaji wa mafuta.

Pia alimwahgiza kuwahamisha askari  ambao ni wataalamu wa kilimo wenye ujuzi wa zao la michikichi kutoka kwenye Magereza mengine mkoani Kigoma  na kuwahamishia katika gereza la Kwitanga ili kuimarisha uzalishaji.

Naye Majuto, Masila alisema ili kilimo cha michikichi na uzalishaji wa mafuta uweze kuwa na tija, wanahitaji wafungwa wasiopungua 300 wawepo kila siku gerezani hapo ili kumudu shughuli za shamba hilo. Kwa sasa kuna wafungwa 112.

“Uzalishaji wa mafuta kwa miaka mitatu mfululizo gerezani Kwitanga ni kama ifuatavyo mwaka 2015/2016 tulizalisha lita 16,094, mwaka 2016/2017 lita 12,674, na mwaka 2017/2018 tulizalisha lita 16,000,”  alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles