31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Ndalichako aipa tuzo Global Education Link

necta.Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, amekabidhiwa tuzo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Kukabidhiwa tuzo hiyo kunatokana na kutambua mchango wa taasisi hiyo katika kuunga mkono sekta ya elimu nchini.

Akikabidhi tuzo hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma, Profesa Ndalichako wakati akifunga mkutano wa tatu wa Maofisa Elimu Mkoa na Wilaya kwa Shule za Msingi na Sekondari (Redeoa), alisema sasa umefika wakati kwa wazazi, walezi na wadau wa elimu nchini kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika sekta ya elimu nchini.

Prof. Ndalichako alisema kwamba, amebaini kuwepo kwa ufisadi katika fedha Sh bilioni 66 zilizotengwa kwa ajili ya mafunzo, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule nchini.

“Hiyo ni ukarabati wa darasa tu la shule za msingi. Wale waliokula fedha hizo nawaambia zitawatokea puani, hatuwezi kuwavumilia watu ambao ni mafisadi wasiokuwa na huruma,” alisema.

Akizungumzia tuzo hiyo Mkurugenzi huyo wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, alisema kukabidhiwa kwa tuzo hiyo ni kama ishara ya kutambua mchango wao kwa Taifa hasa katika kuunga mkono sekta ya elimu nchini.

Alisema hatua ya maofisa elimu wa mikoa na wilaya kukutana pamoja ni sehemu ya kutambua juhudi zao za kusimamia elimu nchini.

“Hawa ndio watendaji wakubwa wa elimu na ndiyo moyo wa elimu nchini na hatua ya Global kuonekana mchango wake ni thamani kubwa kwetu na kwa Taifa letu ni hakika tutaendelea kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono hatua ya Serikali ya kuimarisha elimu,” alisema Mollel.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Redeoa, Juma Kaponda, alisema hatua ya kampuni hiyo ni kuungwa mkono na kila mdau wa elimu nchini.

“Global ni mdau mkubwa wa elimu nchini na kwa mwaka wa tatu mfululizo amekuwa wakituchangia hasa katika mikutano yetu ambapo kwa mwaka huu amechangia shilingi milioni 54 na hakika huu ni mfano wa kuigwa,” alisema Kaponda.

Licha ya hali hiyo alishauri walimu wa shule za msingi waimarishwe kwa maarifa na lugha ya Kiingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles