28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda azindua jengo la upasuaji Mwananyamala

1Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa mteule wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amezindua ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya utoaji wa huduma za upasuaji kwa wajawazito na wagonjwa wengine wadharura.

Jengo hilo ambalo ujenzi wake utaanza rasmi kesho, litakuwa na vyumba maalumu kwa ajili ya upasuaji, uangalizi maalumu kwa ajili ya wagonjwa wadharura (ICU) na uangalizi baada ya upasuaji na vingine kwa ajili ya utawala na huduma nyinginezo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam juzi, Makonda alisema kuwa jengo hilo litakuwa mahususi kwa ajili ya kupunguza idadi ya wagonjwa ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Kupitia jengo hili wajawazito wote na wagonjwa wengine ambao wanahitaji upasuaji watapatiwa huduma hiyo hapa Mwananyamala.

“Jengo hilo litakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa 350-360 hivyo kwa kiasi kikubwa tutakuwa tumepunguza msongamano Muhimbili.

“Pia tutakuwa tumefanikiwa kuokoa maisha ya wajawazito ambayo yamekuwa yakipotea kutokana na kuchelewa kupata tiba,” alisema Makonda.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Azizi Msuya, alisema jengo hilo litasaidia  kuokoa maisha ya wajawazito na wagonjwa wengine ambao wamekuwa wakifariki kutokana na kucheleweshewa kupata huduma hizo.

“Katika wajawazito 100,000 wanaojifungua 447 wanapoteza maisha. Sasa kupitia uwepo wa huduma ya upasuaji katika hospitali hii ya Mwananyamala tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuokoa maisha ya wajawazito hao wanaofariki,” alisema Dk. Azizi.

Mwakilishi wa Kampuni ya GSM Foundation ambao ndio wafadhili wa ujenzi wa jengo hilo, Deogratias Ndejembi, alisema kampuni hiyo imeamua kufadhili ujenzi huo ili kuokoa maisha ya Watanzania ambao wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya upasuaji na pia kutokana na nakuguswa na juhudi za Makonda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles