20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Etihad yajizatiti kwa usalama wa ndege

EtihadABU DHABI, UAE

SHIRIKA la Ndege la Etihad limejizatiti kuimarisha usalama wa ndege kwa kukiimarisha chuo chake cha mafunzo ya urubani kilichopo mjini Al Ain.

Kupitia mpango huo, imekiongezea chuo cha shirika hilo ndege mbili aina ya EA 330 LT zitakazotumika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa marubani juu ya kuhakikisha usalama wao, abiria na ndege.

Ndege hizo zilisafirishwa na kuunganishwa na wataalamu wake katika chuo hicho na zitashiriki maonyesho ya ndege ya Abu Dhabi baadaye wiki hii.

Ndege hizo za nyongeza zitatumika kwa mafunzo yatakayowapa marubani utaalamu wa kutambua, kuzuia hatari ikiwamo kuirudisha ndege katika hali ya kawaida litokeapo tatizo au wakati inapopoteza mwelekeo.

Makamu wa Rais wa Etihad wa Kitengo cha Mafunzo, Christopher Ranganathan, alisema dhumuni kubwa la mafunzo hayo ni kuwapa marubani uwezo wa kuhakikisha usalama na ufanisi katika kazi yao.

Alisema ongezeko la ndege hizo kuungana na nyingine 19 Cessna 172S na Diamond DA4242 ni msaada mkubwa katika kutimiza lengo hilo.

Chuo cha Etihad kinaendesha programu za mafunzo ya leseni ya urubani kufunza raia 120 wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) na wanafunzi wa kimataifa kila mwaka kutoka Etihad na washirika wake, ambao ni mashirika ya ndege ya Alitalia na Shelisheli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles