24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Nchi 14 kushiriki Maonyesho ya Sabasaba

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Jumla ya nchi 14 zimethibitisha kushiriki maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu kama sabasaba ambapo kampuni za ndani zilizothibitisha ushiriki ni 1,188 na kampuni 112 za nje.

Maonyesho hayo yanatarajiwa kuzana kuanza Juni 28 hadi Julia 13, mwaka huu.

Akizungumza Mei 19, na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Biashara TanTrade, Fortunatus Mhambe amesema maonyesho hayo yatakuwa na maeneo mbalimbali yaliyoboreshwa na program za kuvutia.

“Kauli mbiu ya mwaka huu ni maonesho haya ni Tanzania ni mahali sahihi pa biashara na uwekezaji na kusisitiza lengo la maonesho hayo ni kuwakutanisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi,” amesema Mhambe.

Amesema wafanyabiashara wanapata fursa ya kutangaza bidhaa na huduma zao na kutafuta masoko.

“Ningependa kuzungumzia kuhusu sabasaba ExpoVillage ambayo ni moja kati ya program za maonesho ya DITF, eneo hili limejitolea kutangaza fursa zilizopo katika sekta ya madini, Tehama, Gesi na mafuta ,siku ya mazingira, sanaa pamoja vijana na wanawake,” amesema Mhambe.

Aidha, amewataka wafanyabiashara wote kushiriki maonesho ya sabasaba pamoja na kutembelea banda maalum la sabasaba expo Village na kuchangamkia fursa zilizopo.

Amesema hiyo ni nafasi nzuri ya kukuza biashara zetu kujenga mtandao wa kibiashara na kuimarisha mchango wetu katika maendeleo ya nchi kwa kushiriki katika maonesho ya sabasaba wanaweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta za kibiashara na uchumi kwa ujumla.

Mhambe amesema Expo Village tunaweza kuonyesha uwezo wetu wa ubunifu na uvumbuzi eneo hili linatoa fursa kwa wajasiriamali hasa vijana na wanawake, kuonyesha talanta zao na kushiriki katika shughuli za biashara, hii ni njia ya kukuza ujasiriamali na kuwapa fursa wadau wote katika sekta ya biashara.

Aidha, amesema miundombinu ya barabara itarekebishwa kabla ya maonyesho hayo na wameingi mkataba wa miaka mitano na DART kwa ajili ya kusafirisha abiria wanaokuja sabasaba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles